The House of Favourite Newspapers

Mamia Wampokea Tundu Lissu Uwanja wa Ndege Dar, Polisi Waweka Ulinzi Mkali – Video

0

MAKAMU Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu amewasili leo Januari 25, 2023 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Ubelgiji.

Lissu mzaliwa wa Kijiji cha Mahambe, Wilaya ya Ikungi, Mkoa wa Singida amepokewa na viongozi na wanachama wa Chadema.

Mamia ya wafuasi wa Chadema wamekusanyika nje ya lango hilo wakiimba na kucheza huku vigoma vikipigwa pamoja na mavuvuzela.

Jeshi la polisi limeimarisha ulinzi na kuhakikisha wafuasi hao hawaingii ndani ya eneo la uwanja na badala yake wanabaki nje ya lango kuu pembezoni mwa barabara ya Nyerere.

Leave A Reply