The House of Favourite Newspapers

Mamia Wamzika Dickson Kagembe, Bukene Tabora

0
Jeneza lenye mwili wa Dickson Kagembe likifunuliwa kwa ajili ya ndugu na jamaa kuaga nyumbani kwao Bukene.

 

MAREHEMU Dickson Kagembe aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akisomea Sheria na baadaye akakumbwa na ugonjwa wa kansa ya damu (leukemia) ulioyachukua maisha yake Jumapili iliyopita katika Hospitali ya Muhimbili, na  kuagwa juzi katika Kanisa Katoliki, Muhimbili, amezikwa jana nyumbani kwao Bukene wilayani Nzega mkoani Tabora.

 

Waombolezaji wakiwa msibani.

 

Dickson alikuwa mwanafamilia wa wafanyakazi wa kampuni ya Global Publishers, tangu Mkurugenzi Mtendaji wake, Eric Shigongo, kukutana naye wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Ocean Road.

 Siku Ambayo Shigongo Aliwakutanisha Wakonta na Dickson

Shughuli ya kuaga mwili wa marehemu ikiendelea.

 

Mamia ya waombolezaji walijumuika na ndugu, jamaa na marafiki katika kumsindikza Dickson kwenye safari yake ya mwisho hapa duniani.

 

Jeneza lenye mwili wa marehemu Dickson Kagembe.

 

Ndugu, marafiki na wanafunzi wenzake walishindwa kujizuia kumwaga machozi kuondokewa na mtu ambaye alikuwa mhimu kwao na familia yake.

 

 

 

Huzuni ikitanda.

Soma na hii==>Dickson Kagembe Aagwa na Mamia, Kuzikwa Bukene Tabora Kesho

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza.

Dickson aliyefariki akiwa na umri wa miaka 32 na ambaye amekuwa akipata matibabu ya ugonjwa huo kwa miaka ipatayo miwili, ameacha mke na watoto watatu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa; jina lake lihimidiwe! Amina.

Waombolezaji wakiwa msibani.

 

Professional Gathering: Dickson Kagembe Alivyosimulia A-Z Kuhusu Aliyoyapitia Kwenye Maisha Yake

Leave A Reply