Man City Kuvunja Rekodi Kwa Grealish

MANCHESTER City wamesema kuwa wanataka kumsajili kiungo wa Aston Villa Jack Grealish na kumfanya kuwa mchezaji ghali zaidi kwenye Ligi Kuu England.Manchester City, Man United na timu nyingine kubwa zimekuwa zikimwania mchezaji huyo mwenye kiwango cha juu sana uwanjani.

 

Man City wamekuwa wakisema kuwa wanataka kumsajili kiungo huyo na kuvunja rekodi ya usajili kwenye Ligi Kuu England ambayo iliwekwa na Paul Pogba ambaye alisajiliwa na Man United kwa kitita cha pauni milioni 89.

 

Villa bado hawajasema kama wanataka kumuuza Grealish, lakini inaelezwa kuwa kama kuna timu itakwenda na kitita cha pauni milioni 100 watamchukua mchezaji huyo.

 

Hata hivyo, Man City wanataka kuanza na ofa ya pauni milioni 80 kwa ajili ya mchezaji huyo lakini wanaamini kuwa ofa hiyo itakataliwa.Kwa sasa mchezaji ambaye amesajiliwa bei ghali zaidi kwenye timu ya Man City ni Ruben Dias ambaye alisajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 64.5.

🔴#LIVE: KESI YA MORRISON NGOMA MBICHI |BILIONI 4 KUMPELEKA LUIS AL AHLY ​| KROSI DONGO…


Toa comment