The House of Favourite Newspapers

Man United Kumuongezea Mkataba Zlatan Ibrahimovic

gettyimages-586901524

KLABU ya Manchester United imesema kuwa itamuongezea kandarasi ya mwaka mmoja mshambuliaji wake mahiri, Zlatan Ibrahimovic kulingana na kauli iliyotolewa na Meneja wa klabu hiyo, Jose Mourinho.

skysports-man-united-premier-league-zlatan-ibrahimovic_3825374Mchezaji huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 35 alihamia Old Trafford katika uhamisho wa bure mwanzoni mwa msimu huu akitokea Klabu ya PSG, akiwa na uwezo wa kuongeza kandarasi hiyo kwa msimu wa pili. Amefunga mabao 17 katika mashindano yote msimu huu.

Mourinho alisema: “Tutaandaa mpango wa kuongeza kandarasi yake kwa mwaka mwimgine. Baadaye anaweza kufanya atakacho.”zlatanibrahimovicmanchesterunitedvmanchesterlzqpkrnkriel

Ibrahimoviv alisema: “Najihisi vyema, nikiwa nitaendelea itakuwa mwaka mwingine.”

Ibrahimovic amefunga mabao 62 katika mechi 116 akiichezea Sweden kabla ya kustaafu katika soka ya kimataifa mnamo mwezi Juni.

Comments are closed.