The House of Favourite Newspapers

Man United Yaitungua Chelsea

MARCUS Rashford, mshambuliaji wa Manchestr United amefunga mabao mawili muhimu yalioivusha timu yake kwenye hatua ya Robo Fainali ya Carabao Cup.
United ilikuwa inamenyana na Chelsea ambapo mchezo ulikuwa na ushindani mwisho wa dakika 90 Manchester ilishinda mabao 2-1.
Rashford alianza kucheka na nyavu dakika ya 23 kwa penalti kabla ya Mitch Batshuayi kusawazisha dakika ya 61 na bao la ushindi  kwa United likafungwa dakika ya 73 kwa mpira uliokufa uliozama mazima nyavuni ulipigwa na Rashford uwanja wa Stamford Bridge.

Comments are closed.