The House of Favourite Newspapers

Man United Yamtengea Dembele Bil 169

0

KLABU ya Manchester United, ina uhakika wa kutoa kiasi cha pauni 60m (Sh bil 169.4)kwa ajili ya kumsajili straika wa Moussa Dembele wa Klabu ya Lyon ya Ufaransa.United imekuwa ikimfuatilia staa huyo zaidi ya miezi 12 sasa na ilituma maskauti wake kwa ajili ya kuangalia uwezo wake na sasa wameridhika.

 

Miezi sita iliyopita maskauti wa Man United walikwenda kumuangalia katika michezo tofauti na kujihakikishia kuwa anawafaa.

 

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solsjkaer anaamini kabisa kuwa staa huyo ndiyo atakuwa mbadala sahihi wa nafasi ya Romelu Lukaku ambaye alitimka kwenye kikosi hicho na kwenda Inter Milan.

 

Hata hivyo, timu ya Lyon ambako Dembele anakipiga msimu ujao haitashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kumaliza nafasi ya saba huku ligi yao ikifutwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.

 

Rais wa Klabu ya Lyon, Jean Michel Aulas alikiri kuwa hawezi kuzuia mchezaji aondoke ndani ya kikosi chake.

 

“Nitapambana kuona naendelea kuwa na wachezaji wangu, lakini wale ambao watataka kuondoka sababu hatushiriki michuano ya Ulaya basi wataenda,” alisema Aulas.

 

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu wa Man United, Ed Woodward alisema timu yake ipo kwenye nafasi nzuri ya usajili licha klabu nyingi kuyumba kiuchumi.

 

“Tunataka kuimarisha timu yetu msimu ujao na tayari tulimwambia Ole tunataka kushinda makombe hivyo ni lazima tujenge timu imara ya kupamba,” alisema mtendaji.

MANCHESTER, ENGLAND

Leave A Reply