The House of Favourite Newspapers

Man Utd Yakamilisha Usajili wa Andre Onana Kwa Pauni Milioni 47.2

0

Manchester United wamekamilisha usajili wa mlinda mlango Andre Onana kutoka Inter Milan kwa kima cha pauni milioni 47.2m.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 27, ametia saini mkataba wa miaka mitano, na chaguo la kuongezwa kwa miezi 12.

Mkataba huo una thamani ya pauni milioni 43.8 pamoja na nyongeza zinazoweza kufikia za pauni milioni 3.4.

Kipa huyo wa zamani wa Ajax anatazamiwa kuungana na kikosi cha United katika ziara yao ya kujiandaa kwa msimu mpya nchini Marekani.

“Kujiunga na Manchester United ni heshima kubwa,” alisema. “Nimejitahidi sana maishani kufikia ufanisi huu, nikikabilianam na vizuizi vingi njiani.

Onana atachukua nafasi ya David de Gea kama mlinda mlango wa kikosi cha kwanza cha United, baada yaMhispania huyo kuondoka mwezi huu wa Julai wakati mkataba wake ulipokamilika baada ya miaka 12 katika klabu hiyo.

“Huu ni mwanzo wa safari mpya kwangu, na wachezaji wenzangu wapya na malengo mapya ya kupigania, alisema Onana.

“Manchester United ina historia ndefu ya makipa mahiri, na sasa nitafanya kila niwezalo kuandikisha historia yangu katika miaka ijayo,”Onana aliongeza.

Onana alicheza chini ya kocha wa United Erik ten Hag kwa kipindi cha miaka saba na nusu huko Ajax, na kushinda mataji matatu ya ligi.

YANGA MPYA ni BALAA, KINATOKA CHUMA KINAINGIA CHUMA/ SIMBA YAZIDI KUSHUSHA MASTAA KIBABE…

Leave A Reply