The House of Favourite Newspapers

MAN WATER AFUNGUKIA KUPOTEA KWA MR NICE, 20 PERCENT

0
Man Water kushoto akiwa na 20 Percent.

MAN Water si jina geni kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva. Hili ni jina la prodyuza na mmiliki wa Studio ya Combination Sound yenye makazi yake mitaa ya Kinondoni, Dar. Lakini pia uzito wa umaarufu wake umeongezeka kutokana na kutengeneza ‘hit song’ kibao kwenye gemu la muziki zikiwemo nyimbo za mkali wa miondoko ya Takeu, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’, kama vile Kikulacho, Kuku Kapanda Baiskeli na nyingine nyingi!

Mbali na kuwa prodyuza Man Water pia ni mtangazaji, na muandaaji wa vipindi vya redio na televisheni, amewahi kufanya kazi katika studio za Chanel Ten na sasa yupo kwenye kituo cha Televisheni cha Azam akiandaa vipindi. Katika makala haya Man Water amefunguka mengi kuhusu kazi zake, alivyochangia kwenye mafanikio ya kina Mr. Nice na 20 Percent na kupotea kwao. Risasi Vibes: Man Water unaweza kuwaeleza wasomaji umeanza gemu la muziki lini? Man Water: Ni muda mrefu sana. Kwa sasa nina miaka kumi na saba hivi kwenye gemu.

Manafungukia kupotea Mr Nice, 20 Percent changamoto ambayo inanifanya nizidi kukomaa siku hadi siku.

Risasi Vibes: Umefanya kazi na Mr. Nice, naweza kusema ni kama ulimtoa kwenye gemu, unafikiri nini kilisababisha apotee?

Man Water: Jibu litakuwa ni lilelile kwamba ilifika wakati akatakiwa kubadilika, nyimbo alizokuwa anaimba zilikuwa ni za kuwateka watoto zaidi lakini baadaye zilionekana si kitu. Kwa hiyo naye muda ulimtupa mkono.

Risasi Vibes: Vipi kuhusu 20 Percent? Inasemekana kupotea kwake kulitokana na wewe na yeye kuwa na bifu?

Mwanamuziki Mr Nice.

Man Water: Sikuwa na bifu na 20. Ni mdogo wangu sana, ila kilichotokea tulitofautiana kwenye kauli. Nakumbuka ilikuwa ni kwenye shoo Morogoro kuna mambo yalitokea nikawa nimeongea naye kwa lugha ya ukali kidogo ili kumuweka sawa kama mdogo wangu. Lakini alichukia tukajibishana na mwisho wa siku ndiyo hivyo hatukuendelea kufanya kazi pamoja. Mbali na hilo kuna sababu nyingine za kimaisha ambazo yeye mwenyewe ndiye anaweza kuzizungumzia zaidi.

Risasi Vibes: Lakini jamaa yupo vizuri, hutegemei kumrudisha? Man Water: Tupo katika jitihada hizo na hivi karibuni 20 atasikika tena.

Risasi Vibes: Vipi kuhusu ndoto zako za kimuziki? Man Water: Nahitaji kufika mbali zaidi, kufanya kazi za kimataifa ndiyo maana nazidi kukomaa.
Risasi Vibes: Wakati unaanza na sasa unaona kuna tofauti gani kwenye muziki?

Man Water: Ni mabadiliko ya muda ambayo ni ya kawaida kabisa. Na hii ni kutokana na kizazi. Muziki umebadilika si kama ambao tulikuwa tunatengeneza huko nyuma, na kazi pia imekuwa na changamoto maana kwa sasa maprodyuza ni wengi kuliko zamani.

Risasi Vibes: Umesema una miaka takribani 17 kwenye gemu, ni muda mrefu sana ukiangalia maprodyuza mlioanza nao kazi kwa sasa wengi wamepotea, unafikiri nini kimewapoteza? Man Water: Kama nilivyosema hapo awali ni mabadiliko ya muda, ambayo yanamtaka prodyuza kufanya kitu husika kulingana na wakati unavyotaka. Na hapo ni kwamba atake ama asitake. Sasa wale ambao waliendelea kushikilia swaga za zamani ndiyo hivyo wanapotea.

Risasi Vibes: Nini hasa siri yako ya kuendelea kudumu kwenye muziki Bongo na wasanii bado kuendelea kufanya kazi na wewe?

Man Water: Najifunza kila siku mambo mapya. Kamwe sidharau hawa maprodyuza wapya kwamba hawajui na sisi ambao tupo tangu zamani tunafahamu zaidi. Kiukweli kwangu wao ni moja ya changamoto ambayo inanifanya nizidi kukomaa siku hadi siku.

Risasi Vibes: Umefanya kazi na Mr. Nice, naweza kusema ni kama ulimtoa kwenye gemu, unafikiri nini kilisababisha apotee?

Man Water: Jibu litakuwa ni lilelile kwamba ilifika wakati akatakiwa kubadilika, nyimbo alizokuwa anaimba zilikuwa ni za kuwateka watoto zaidi lakini baadaye zilionekana si kitu. Kwa hiyo naye muda ulimtupa mkono.

Risasi Vibes: Vipi kuhusu 20 Percent? Inasemekana kupotea kwake kulitokana na wewe na yeye kuwa na bifu?

Man Water: Sikuwa na bifu na 20. Ni mdogo wangu sana, ila kilichotokea tulitofautiana kwenye kauli. Nakumbuka ilikuwa ni kwenye shoo Morogoro kuna mambo yalitokea nikawa nimeongea naye kwa lugha ya ukali kidogo ili kumuweka sawa kama mdogo wangu.  Lakini alichukia tukajibishana na mwisho wa siku ndiyo hivyo hatukuendelea kufanya kazi pamoja. Mbali na hilo kuna sababu nyingine za kimaisha ambazo yeye mwenyewe ndiye anaweza kuzizungumzia zaidi.

Risasi Vibes: Lakini jamaa yupo vizuri, hutegemei kumrudisha?

Man Water: Tupo katika jitihada hizo na hivi karibuni 20 atasikika tena.

Risasi Vibes: Vipi kuhusu ndoto zako za kimuziki?

Man Water: Nahitaji kufika mbali zaidi, kufanya kazi za kimataifa ndiyo maana nazidi kukomaa.

NA: BONIPHACE NGUMIJE 

Leave A Reply