The House of Favourite Newspapers

Manara Amaliza Msala Wake TFF

0

OFISA Habari wa Simba, Haji Manara, jana Jumatano mchana, alifika kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulipa faini ya Sh milioni tano ambayo alitozwa na Kamati ya Maadili ya TFF.

 

Hivyo kwa sasa hana msala tena.Manara amechukua uamuzi huo wa haraka baada ya Jumatatu ya wiki hii, Kamati ya Maadili ya TFF kumtoza faini hiyo pamoja na viongozi wengine watatu.

 

Manara alikutwa na hatia kwa kuingilia majukumu ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji wakati wa kesi ya mchezaji Bernard Morrison raia wa Ghana.

Wengine waliotozwa faini ni Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli na Mjumbe wa Kamati ya Sheria ya TFF, Zakaria Hanspope.

 

Wote hao hukumu yao ilitoka kutokana na sakata la Morrison.Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF, Wakili Kichere Mwita Waissaka, amesema kwa wasioridhika na uamuzi huo uliotolewa Jumatatu ya wiki hii, rufaa ipo wazi ambapo Hanspope amepanga kukata rufaa mara tu atakapopokea nakala ya hukumu hiyo.

Leave A Reply