The House of Favourite Newspapers

Barbados Kumuondoa Malkia Elizabeth Kama Mkuu wa Nchi

0

VISIWA wa Barbados vimetangaza nia yake ya kumuondoa Malkia Elizabeth kama kiongozi wa nchi hiyo na kuwa Jamuhuri.

 

”Muda umewadia wa kuachana na historia yetu ya kikoloni,” Serikali ya taifa hilo la kisiwa hicho cha Caribbean imesema.

 

Ina lengo la kumaliza mchakato huo wakati wa kumbukumbu ya miaka 55 ya uhuru wake kutoka Uingereza, itakayofanyika mwezi Novemba mwaka 2021. Hotuba iliyoandikwa na Waziri Mkuu, Mia Mottley, imesema raia wa visiwa hivyo wanamtaka kiongozi mzawa.

 

Kasri la Buckingham lilisema kuwa HILO ni suala la serikali na watu wa visiwa vya Barbados. Chanzo cha habari katika kasri la Buckingham kimesema kuwa wazo hilo ”halikuja tu ghafla” na ” limekuwa likizungumzwa hadharani mara nyingi”, Mwanahabari wa BBC, Jonny Dymond, alisema.

 

Kuhusu Barbados:

  • Moja kati ya visiwa maarufu katika Caribbean
  • Ilipata uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1966
  • Malkia Elizabeth ameendelea kuwa mtawala wa kikatiba
  • Inajitegemea sana katika uchumi utokanao na shughuli za usafirishaji wa sukari, pia kwenye utalii
  • Waziri Mkuu wake ni Mia Mottley, alichaguliwa mwaka 2018 na mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.

 

Kauli hiyo ilikuwa sehemu ya taarifa ya serikali ya kifalme, ambayo imetanabaisha sera za serikali na programu katika kuelekea vikao vipya vya bunge. Wakati ikisomwa na gavana mkuu, ina maana kuwa imeandikwa na waziri mkuu wa nchi.

Hotuba hiyo pia ilinukuu onyo kutoka kwa Errol Barrow, Waziri Mkuu wa kwanza wa Barbados baada ya kupata uhuru, ambaye alisema kwamba nchi hiyo haipaswi “kurandaranda kwenye maeneo ya majengo ya wakoloni”.

 

Sio sauti yake tu huko Barbados ambayo imekuwa ikipendekeza kuhama kutoka kwenye utawala wa kifalme. Tume ya ukaguzi wa katiba ilipendekeza hadhi ya jamhuri kwa Barbados mnamo 1998.

 

Mtangulizi wa Bi Mottley katika nafasi hiyo, Freundel Stuart, pia alitetea “kuhama kutoka kwa mfumo wa utawala wa kifalme kwenda kwa serikali ya jamhuri katika siku za usoni”.

 

Barbados haitakuwa koloni la kwanza la Uingereza katika Carribean kuwa jamhuri. Guyana ilichukua hatua hiyo mnamo 1970, chini ya miaka minne baada ya kupata uhuru kutoka kwa Uingereza. Trinidad na Tobago walifuata nyayo mnamo 1976 na Dominica mnamo 1978.

 

Wote watatu wamekuwa ndani ya Jumuiya ya Madola, umoja wa nchi huru za makoloni ya zamani ya Uingereza pamoja na nchi nyingine ambazo hazina mafungamano ya kihistoria na Uingereza.

 

Ni jambo lisilo la kawaida kwa nchi kumuondoa Malkia kama kiongozi wao. Nchi ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa Mauritius mwaka 1992. nchi nyingine za Caribbean kama vile Dominica, Guyana, Trinidad na Tobago zilikuwa jamuhuri katika miaka ya 1970.

 

Nchi 15 ambazo ni sehemu ya dola ya Malkia zinaonekana kuthamini mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo na Uingereza. Ni kweli, baadhi wamekuwa wakiongelea suala ya kuwa na wakuu wao wa nchi na kuachana na utawala wa kifalme. Lakini mara nyingi malengo ya kisiasa yamekuwa kikwazo.

Si mara moja kwa wanasiasa wa Barbados kueleza nia yao ya kuwa Jamuhuri. Swali ni kuwa kama uamuzi huu utalingana na wengine. Jamaica awali alisema kuwa hiyo ni njia ambayo ingeifuata. Umuhimu wa jambo hili unaelezwa kuwepo katika suala la kuondokana na ‘historia ya kikoloni’.

 

Katika dhana ya kampeni ya Black Lives Matter, itakuwa jambo linalosubiriwa kuona kama hatua hii italeta msukumo wa kisiasa kwa serikali za Caribbean kuchukua mkono huo huo.

 

Na ikiwa hili litatokea, na kuondolewa kwa Malkia kama mkuu wa nchi kutlingana na, tuseme, kuondolewa kwa sanamu ya mfanyabiashara wa watumwa, basi hiyo inaweza kusababisha maswali magumu kwa familia ya kifalme ya Uingereza na Jumuiya ya Madola.

Leave A Reply