The House of Favourite Newspapers

Manara Atembelea Shule Aliyosoma, Aibua Hili

0

MSEMAJI wa Klabu ya Simba, Haji Manara ametembelea Shule ya Sekondari Chimala iliyopo Mkoa wa Mbeya ambayo alisoma miaka kadhaa iliyopita wakati akijipatia elimu yake ya sekondari.

Baada ya kufika shuleni hapo, Manara alipata fursa ya kukutana na wanafunzi wa shule hiyo wanaosoma hapo kwa sasa na kuzungumza nao pia akazungumza na walimu wa shule hiyo kuhusu mambo machache waliyoweza kujadili.

Aidha, Manara alitembelea mabweni na kitanda alicholalia wakati akisoma huku pia akitembelea madarasa na hali ya Ukumbi Mkuu wa shule hiyo ambayo amedai yapo kwenye hali mbaya tofauti na ilivyokuwa miaka hiyo ambayo wao walikuwa wakisoma.

Manara amesema kwamba atafanya mkakati wa kuzungumza na wanafunzi wenzake aliyosoma nao shuleni hapo ili waufanyie ukarabati.

 

Manara amesema; “Jana nilibahatika kutembelea shule niliyosoma Sekondari, Chimala Secondry Sschool iliyopo mkoani Mbeya. Nilifurahi na kuhuzunika pia baada ya kuona hadi kitanda nilicholalia miaka kadhaa iliyopita bado kipo vile vile.

“Jiko na mabweni halikadhalika, hali ya madarasa na Ukumbi mkuu wa shule ni mbaya kuliko ilivyokuwa zamani.

“Nimechukua hatua kadhaa na nitawashirikisha wenzangu niliosoma nao pamoja na rafiki zangu wa karibu angalau kuiweka katika mazingira rafiki, shule ya maisha yangu. Muhimu sana kukumbuka tulipotoka ili tusisahau tunapotaka kwenda kunafananaje,”amesemaManara.

Leave A Reply