The House of Favourite Newspapers

Manara: Mwisho wa Kumsajili Mchezaji ni 230m

0

MSEMAJI Mkuu wa Simba, Haji Manara amebainisha kwamba ni ngumu kwa klabu hiyo na nyingine za Tanzania kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu wanasajili mchezaji mwisho kwa dola laki moja (Tsh 230,409,000) wakati wenzao wanaweza kusajili hadi kwa dola laki nane (Tsh 1,843,270,000).

 

Manara ameweka bayana kwamba kwa klabu za hapa kuna uwekezaji mdogo ikiwa ni tofauti na timu nyingine za Afrika kama Al Ahly ya Misri ambao wamekuwa na uwekezaji mkubwa.

 

Manara amesema kwamba kutokana na uwekezaji huo ndiyo maana inasababisha kwao na klabu nyingine kushindwa kutwaa ubingwa huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika na mataji mengine.

 

“Hatuwezi kununua mchezaji wa dola laki 5 lakini wenzetu wanaweza kufanya kitu kama hicho. Kwetu mchezaji mkubwa zaidi ni dola laki au laki na ishiriki lakini Al Ahly wanatoa dola milioni nane.

 

“Uwekezaji wetu ni mdogo, huwezi kuchukua ubingwa wa mataji makubwa kwa uwekezaji huu, bado hatujawa tayari kwa sababu uwekezaji wetu mdogo. Bingwa kutoka Tanzania kwa uwekezaji wetu hatuwezi lakini inaweza kutokea ‘kufurukuta’ ukachukua kikombe lakini wenye chao msimu ujao wakachukua lakini kuwa bingwa wa kila mara kwa hapa bado,” alisema Manara.

Mwandishi Wetu

Leave A Reply