MANARA: SIMJUI AFANDE SELE, KULA TU TABU, ANAROPOKA – VIDEO

BAADA ya kutokea sintofahamu kutokana na masuala ya ushabiki wa Simba na Yanga, Rapa maarufu nchini, Selemani Nyandindi maarufu kama ‘Afande‘ au Mkali wa Rhymes hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Facebook alimtolea maneno makali Msemaji wa Simba, haji Manara jambo ambalo naye amejibu mapigo.

 

Manara amesema hamjui Afande Sele wala hawezi kumzungumzia; “Kuna watu zama zao zikishaisha lazima watafute pakutokea, nani anamjua huyo mtu? Huyo msanii mimi hata simjui, ninawafahamu wasanii wakubwa akina Prof. Jay, Sugu, Alikiba, Diamond, Jay Dee na wengine ambao wamefanya mambo makubwa.

 

“Nani anamzungumza huyo mtu, kumzungumza ni kujishuhsia heshima, anatapatapa, anasubiri Israel aje afanye yake, hata kula tu anapata shida, mimi nashughulikia mambo makubwa wala sio rabishi za mtaani, acha wamshughuliki huko mitandaoni,” amesema Manara.

 

Mvutano huo unadaiwa kusababishwa na mjadala wa kugombea wachezaji wa kimataifa akiwamo Raia wa Rwanda Haruna Niyonzima.

MSIKIE MANARA AKIMCHANA AFANDE

Loading...

Toa comment