The House of Favourite Newspapers

Manchester City Yaichapa PSG 2-1 Nusu Fainali UEFA

0

MANCHESTER City imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya PSG katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kwanza ya UEFA Champions League.

 

Ni Marquinhos wa PSG alipachika bao pekee kwa timu hiyo inayonolewa na Mauricio Pochettino lilidumu mpaka muda wa mapumziko.

 

Vijana wa Pep Guardiola warirejea kipindi cha pili kwa kasi na dakika ya 61 Kevin de Bruyne alipachika bao la kuweka mzani sawa kisha Riyad Mahrez alimaliza kazi dakika ya 71 kwa pigo huru na kuwapa mzigo PSG kusaka ushindi katika mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Mei 4 Uwanja wa City of Manchester.

Idrissa Gueye wa PSG dakika ya 77 alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea faulo IIkay Gundogan na kuwafanya vijana wa Pochettino ndani ya Uwanja wa Parc des Princes kuwa pungufu ndani ya uwanja.

 

Pochettino amesema kuwa wachezaji wake walishindwa kuumudu mchezo huo kwa kuwa walicheza bila nguvu katika kutafuta matokeo na hata walipokuwa na mpira hawakuonyesha jitihada.

 

“Nadhani kwamba wachezaji walishindwa kuwa na nidhamu jambo ambalo lilifanya tukapoteza mchezo wetu, pia hata pale ambapo walikuwa wakipata mpira umiliki wao ulikuwa hauna nguvu kubwa.

 

“Manchester City wameweza kuwa na nidamu na kuonyesha utofauti, nadhani kuna jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi kwa ajili ya wakati ujao,” .

Leave A Reply