The House of Favourite Newspapers

Maneno ya Schweinsteiger Baada ya Mourinho Kumrejesha Kikosini

united_captain_wayne_rooneyManchester: IKIWA ni siku moja tu baada ya Kocha Jose Mourinho kumrudishwa kikosini na kuanza kufanya mazoezi kwenye kikosi cha kwanza cha Klabu ya Manchester United, Mjerumani, Bastian Schweinsteiger ameandika ujumbe wa kuwatia moyo mashabiki wa timu hiyo.

Akiandika kupitia ukurasa wa Instagram, kiungo huyo ameandika, “Felt great today! Team is in good shape, results will follow! @manchesterunited.”

Staa huyo amekuwa na wakati mgumu ndani ya Mashetani Wekundu chini ya kocha Mreno, Jose Mourinho akiwa mpaka sasa hajacheza mechi hata moja tangu msimu ulipoanza mwezi Agosti, mwaka huu.

Mara ya mwisho nahodha huyo wa zamani wa Ujerumani kuchezea timu yake hiyo ya United ilikuwa ni msimu uliopita wa mwezi Machi, mwaka huu akiwa chini ya kocha Louis Van Gaal aliyetimuliwa kabla ya ujio wa Mourinho klabuni hapo ambaye awali alimkataa Schweinsteiger lakini kwa sasa anaonekana mchango wake kwenye klabu hiyo unahitajika.

Comments are closed.