MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yusuf Manji ameachiwa huru katika kesi ya madawa iliyokuwa ikimkabili baada ya mahakama kushindwa kuthibitisha madai hayo.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Cyprian Mkeha alitumia zaidi ya saa moja kusoma hukumu hiyo akiichambua kesi tangu mshitakiwa huyo alivyokamatwa mpaka alivyochukuliwa kipimo cha mkojo.
Baada ya kueleza hayo hakimu huyo aliuchambua ushahidi uliotolewa kwa pande zote mbili ambapo alihitimisha kwa hukumu ya kumuachia huru mshitakiwa.
Hukumu mhiyo ilizua mayowe ya furaha na kukumbatiana kwa kupongezana ambapo mahakama hiyo iligubikwa na furaha kila kona.
Manji baada ya kuachiwa huru wanahabari walitaka kuzungumza naye lakini watu wake wa karibu walimzuia kufanya hivyo na kumkimbiza kwenye gari na kumuondoa eneo hilo.
Kufuatia hukumu hiyo mwanahabari wetu alizungumza na wakili wa Serikali aliyekuwa akisimamia kesi hiyo, Nassoro Katuga na kutaka kujua wanavyoipokea hukumu hiyo.
“Ukweli sisi hatukubaliani na hii hukumu ni lazima tukate rufaa kwani mahakama imetupa siku 30, za kukata rufaa kama hatukubaliani na hukumu.
Hivi unavyotuona tunasubili nakala ya hukumu ili tuanze mchakato wa kukata rufaa.
Manji alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 akituhumiwa kwamba, kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View, Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroine.
Manji ambaye alikuwa mshtakiwa alikuwa na mshahidi 7 wakati upande wa mashtaka ulikuwa na mshahidi watatu.
PICHA NA RICHARD BUKOS NA DENIS MTIMA | GPL