The House of Favourite Newspapers

Manji Akwama Tena Mahakama Kuu

0
Manji akifikishwa kortini.

Manji akwama tena mahakama kuu

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya kupewa dhamana kwa mfanyabiashara maarufu nchini na aliyekuwa Mweyeiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji.

 

 

Manji aliwasilisha mahakamani hapo maombi ya kupewa dhamana lakini imeshindikana na sasa amerejeshwa rumande.

manji akwama tena mahakama kuu

 

Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe, plate number mbili za magari ya serikali.

 

Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja na wote wamerudishwa rumande.

 

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

LIVE: Rais Magufuli Akiwahutubia Wananchi wa Korogwe – Tanga

Leave A Reply