Manji Anyang’anywa Shamba na Serikali

Yusuf Manji.

SERIKALI imelifuta shamba la mfanyabiashara Yusuf Manji lililopo Kigamboni, lenye ukubwa wa eka 714. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema leo Jumatano kuwa, shamba hilo litapangiwa matumizi mengine.

Lukuvi amesema shamba lingine la Kampuni ya Amadori lenye ukubwa wa eka 5,400 pia limefutwa. Waziri amesema mashamba hayo sasa yako mikononi mwa Serikali na yatapangiwa matumizi mengine.

Lukuvi amewaonya wananchi wasivamie maeneo hayo kwa kuwa watakaokamatwa  watashitakiwa. “Muyaache maeneo hayo kama yalivyo mkijenga tutakuja kuvunja,” amesema.

Jambazi Aliyeongoza Mauaji ya Polisi 8 Kibiti Auawa -Dar


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Loading...

Toa comment