The House of Favourite Newspapers

Manny Pacquiao Kuwania Urais Ufilipino

0

BONDIA mashuhuri wa Ufilipino, Emmanuel Dapidran Pacquiao maarufu kama ‘Manny Pacquiao’ ametangaza leo kuwa atawania kiti cha urais kwenye uchaguzi wa mwaka unaokuja, uamuzi unaohitimisha fununu za miezi kadhaa juu ya iwapo angegombea wadhifa huo wa juu nchini Ufilipino.

 

Katika hotuba yake ya kukubali uteuzi wa kuwania urais kupitia kundi hasimu ndani ya chama tawala cha Rais Rodrigo Duterte, Pacquiao amesema wakati umewadia wa kushiriki kwenye kinyang´anyiro cha uongozi.

 

Pacquiao ambaye alijiunga na siasa mwaka 2010 baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge na baadae seneta, ametarajiwa kwa muda mrefu kutangaza nia yake ya kugombea urais nchini Ufilipino.

 

Rikodi yake kwenye mchezo wa ndondi pamoja na ajenda yake ya kupambana dhidi ya umasikini na rushwa vinatarajiwa kuwa turufu muhimu kwenye kampeni yake katika uchaguzi wa mwaka 2022.

 

Leave A Reply