The House of Favourite Newspapers

’Mapacha’ Wanaosumbua Kwenye Gemu Bongo!

0

heres-what-students-learn-in-a-college-course-on-kanye-west-and-jay-zs-relationship Jay Z na Kanye

BONIPHACE NGUMIJE

Ukiachilia kuunda makundi ya muziki, ‘Chemistry’ ni moja kati ya vitu muhimu kufanywa na wasanii maana huwasaidia kukusanya mashabiki wengi kwa wakati mmoja.

Wale wanaomkubali mmoja wao wanapata nafasi ya kumsikiliza huyo pacha wake kwenye kazi, jambo ambalo linafanywa na wasanii wengi wa kimataifa na duniani kote.

Ukicheki Mamtoni, mambo ni kama hivyo. Jay Z na Kanye waliwahi kuungana wakatengeneza ngoma kali zikiwemo Otsis na Nigaz in Paris.

eminem-and-dr-dreEminem na Dk. Dre

Mashabiki wao wote wakaungana kufuatilia kazi zao, upande mwingine Eminem akapiga kazi na Dk. Dre kwenye ngoma kama vile Guilty Conscience, Forgot About Dre na I Need A Doctor.

Kibongobongo pia wapo wasanii ambao waliungana, wakatoka ngoma kali ile mbaya. Hawa hata leo hii wakifanya kazi pamoja lazima kitoke kitu ‘amaizing’.

fa na ayAy na FA

Ukaribu wao ulianza kitambo kipindi wakiwa ndani ya Kundi la East Coast Team ambapo hata walipomeguka ndani ya kundi hilo bado waliendelea kuambatana kama kumbikumbi.

Mashabiki wa wasanii hawa watakuwa wanawakumbuka vyema kwenye ngoma za Usije Mjini na Habari Ndiyo Hiyo lakini pia mbali na nyimbo hizo wamekuwa wakishirikishana kwenye video zao hata kwa kuuza sura tu. Mfano: AY ameonekana kwenye video ya FA iitwayo Mfalme.

temba na cheggeTemba na Chegge

Hawa ni mapacha wengine kwenye gemu la muziki Bongo. Ni nadra kusikia ngoma mbili za Chegge zimetoka bila sauti ya Temba.

chege na tembaKama ilivyo kwa AY na FA, hawa pia walifahamika kwenye gemu wakiwa pamoja kwenye kundi moja la Wanaume Family alilokuwepo pia Juma Nature.

Miongoni mwa ngoma walizoshirikiana ni Lover Boy, Nikiss Nikukiss ambao wamemshirikisha pia Ommy Dimpoz na Kaunyaka waliomshirikisha Mapolosa kutoka Afrika Kusini.

mesen na pam dPam D na Mesen

Ukiachilia mbali uhusiano wao wa kifamilia, Pam na Mesen wanatengeneza ‘Chemistry’ nzuri sana. Pam D amewahi kusikika akisema huhisi kuwa huru na mwenye raha anapopiga mzigo na Mesen akimaanisha katika kuandaa nyimbo na kuburudisha. Ngoma walizorekodi pamoja ni Nikikupata na Popolipopo.

amin na bekaAmini na Barnaba

Gemu lilianza kuwatambua kupitia Jumba la Vipaji Tanzania (THT), kila mmoja wao akikimbiza kutokana na aina ya uimbaji wake hasa kwenye suala zima la nyimbo za mahaba za kubembeleza.

Ni muda sasa wamekaa kimya bila kushirikiana kwa kufanya kolabo pamoja, lakini ‘Chemistry’ yao ilikuwa pouwa sana hasa tukirejea nyimbo za Mbalamwezi na Why Me walizopiga pamoja.

NaywamitegoftDiamondMuzikiGaniiiiDiamond na Nay wa Mitego

Wote ni wakali, wana mashabiki wengi kwenye tasnia ya muziki ndani na nje ya Bongo. Chemistry yao imekuwa ikipendwa na mashabiki wao kwani wanafanya vizuri sana.

Leave A Reply