The House of Favourite Newspapers

Mapazia ya Chumbani -16

…alichokifanya alivua nguo zote kisha akachukua simu na kutuma meseji kwa mama Muro na mwenzake.
‘Njooni hadi sebuleni mlango upo wazi!’
ENDELEA NAYO MWENYEWE…

“Nikwambie kitu,” alisema mama Kirumba baada ya kuzidiwa utamu wa mwanzo.Msimamo wa yule kijana ni kutosema neno lolote kutokana na sauti yake ingetambulika kama siyo mzee Mashali na mtego kuumbuka.

“Si naongea na wewe jamani, maana hata sauti hutaki kuitoa leo au kuna tatizo?”
“Hakuna tatizo,” yule kijana aliamua kufungua kinywa chake na kuitoa sauti ya kunong’oneza. Mama Kirumba akashtuka!
“Unasema?”

“Hakuna tatizo mpenzi,” yule kijana akairudia tena sauti ile ya kunong’oneza.
Mama Kirumba akawa ameamini moja kwa moja mzee Mashali hayuko vizuri kiafya.
“Basi tuendelee mpenzi.”

Ndani ya dakika chache ungwe ya kwanza ikawa imeshakamilika.
“Bebi leo umeniweza kweli,” alisema mama Kirumba.
“Nimekuweza kivipi mpenzi?” aliongea kwa sauti ileile ya kunong’oneza.
“Leo umenipa mahaba, yaani hadi naiona sakafu ya moto, kuna kipindi nilitamani risasi zisitoke kabisa kwenye hiyo bunduki yako.”
“Kweli?”

“Kweli, japokuwa umebanwa na kifua lakini umepiga mzigo wa ukweli, ama kweli mama Dick anafaidi sana,” mama Kirumba aliendelea kumsifu yule kijana bila kutambua kuwa siye mzee Mashali aliyemdhania.

***

Si mama Dick wala mama Muro kila mmoja alikuwa na shauku ya kwenda kummaliza mama Kirumba. Dukuduku la muda mrefu lilikuwa limemkaba sana mama Dick.

“Mama Muro, embu twende sasa taa si uliziona zimezimwa muda mrefu.”
“Ndiyo lakini yule kijana na yeye si mwanaume, acha kwanza ajimegee.”
“Twende bwana,” alisisitiza mama Dick.

“Si alikutumia meseji kuwa mlango upo wazi tuingie tu?”
“Ndiyo na ninavyomjua mama Kirumba alivyo mpenda sifa yule, atakuwa anaburutana na huyo kijana nyumba yote akidhania yupo na mzee Mashali.
“Embu acha kunichekesha na kunipa hasira,” alisema mama Dick.
Hatua kadhaa ziliwatosha mama Muro na mama Dick kufikia nyumba ya mama Kirumba.

“Si unaona, yule kijana mjanja wa mjini ona mlango alivyoufungua na kuuacha wazi kimtego, tuingie sasa.”
“Mama Muro, tuingie moja kwa moja tutajua wapo upande gani?”
“Si chumbani?”

“Mh, kama wapo sehemu nyingine labda jikoni halafu tukaenda chumbani si tutakuwa tumeharibu?”
“Haya mpigie simu?”

“Simu tena? Hapana tutaharibu zaidi.”
“Sa tutafanyaje tumuingilie moja kwa moja basi.”
“Nina wazo!”
“Wazo gani?”

“Tuingie kwa taratibu tukinyata huku tukisikia sauti zao zitakapotokea, najua mama Kirumba hawezi kutoa sauti ndogo,” alisema mama Muro.
Walifanya hivyo, walianza kupiga hatua moja kwenda nyingine wakinyata, wakasikia sauti ya miguno ya kimahaba.
“Ohh, jamani bebi, nipe yote achana na mama Dick.” Ilisikika sauti ya mama Kirumba sebuleni.

Mama Muro na mama Dick wakapiga breki, hasira kali zilimkaa mama Dick baada ya kuyasikia maneno yale kutoka kwa mama Kirumba. Wakasogea hadi karibu na kuwasha taa.
“Kwisha habari yako!”
Sauti ya mama Muro ikatoka baada ya taa kuwashwa na mama Dick. Mama Kirumba alibaki na mshangao, aligeuza macho yake na kuona vitu ambavyo hakutarajia.
“Endelea sasa na maneno yako,” aliropoka mama Muro.

Bado mama Kirumba alishikwa na kigugumizi, alimuangalia mama Dick kwa muda mrefu kisha akamgeukia yule kijana.
“Ulidhania ndiyo mume wangu uliyezoea kujizolea tu utakavyo enhh,” aliongea mama Dick kwa sauti ya hasira.

“Hapana jamani kwani nini?”
“Uliyekaa naye hapo chini kama ulivyozaliwa unajua ni nani?”
“Huyu?”

“Kwani tunamzungumzia nani?”
“Huyu si…”
“Sema nani?
“Huyu ni mchumba wangu.” Maneno yale yalimpandisha hasira zaidi mama Dick, akampa vibao vya nguvu.

Mama Kirumba akaanza kuangua kilio cha uongo na kweli, yule kijana akainuka na kuvaa nguo zake. Mama Muro na mama Dick wakaweka kanga zao vizuri kiunoni kila mmoja akaanza kumshambulia mama Kirumba kwa kumkwarua na makucha pamoja na kumvuta maziwa yake.

Mama Muro aliitoa ile simu na kumuonesha meseji zote kuwa ni mtego waliomfanyia.
“Naombeni msamaha sitarudia tena jamani!” alisema mama Kirumba.
“Kwa nini unichukulie mume wangu,” alisema mama Dick kwa sauti ya kulia.
“Alikuja kuniuzia mapazia.”
“Ikawaje?”

“Akanifungia chumbani.”
“Halafu?”
“Tukajikuta tukifanya, jamani nisameheni, nimekosa mimi, nimekosa sana.”
Roho ya huruma ikamtembelea mama Dick, akaacha kumpiga na kujutia kitendo cha mumewe kujiingiza katika biashara ya kuuza mapazia.

Kesho yake akamsimulia mumewe kila kitu kilichotokea usiku, akamuomba msamaha na kuirudia kazi ya gereji.
MWISHO.

Comments are closed.