The House of Favourite Newspapers

MAPENZI SIYO KIPAUMBELE KWA DIANA

Diana Kimari

MREMBO wa Bongo Movies, Diana Kimari amesema kuwa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi, lakini hautilii maanani uhusiano wake huo kwani siyo kipaumbele chake.  

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Diana alisema akiamua kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na kuutilia maanani anaona kuna vitu vingine anaweza asivifanye wakati bado ana mambo mengi ya kufanya.

 

“Siyo kwamba sina mpenzi, bali sijamchukulia kihivyo huyo mwanaume kwa sababu naona kuna vitu vingine vya kufanya hivyo akili yangu yote nikiipeleka huko itakuwa ni tatizo, ndiyo maana sitaki hata kumuonesha mahali popote kwa sasa,” alisema Diana bila kutaja mambo hayo mengine yanayomfanya awe bize.

Stori: Imelda Mtema, Dar

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.