Mapinduzi Cup kazi inaanza Leo Alhamisi Uwanja wa Amaan, Zanzibar
LEO Alhamisi kwa maana ya Desemba 28, 2023, michuano ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuanza kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Michuano hiyo ambayo bingwa mtetezi ni Mlandege ya Zanzibar, inatarajiwa kufanyika kwenye viwanja viwili, Amaan uliopo Unguja na Gombani kule Pemba.
Kwa msimu huu, jumla ya timu 12 zinatarajiwa kushiriki zikiwa zimepangwa kwenye makundi matatu. Kila kundi linaundwa na timu nne ambapo timu mbili za juu katika makundi, zitafuzu moja kwa moja robo fainali, kisha ‘best looser’ wawili wataungana nao kukamilisha timu nane.
Mchezo wa ufunguzi utakuwa ni mabingwa watetezi, Mlandege watakaocheza dhidi ya URA kutoka Uganda, kisha baadaye, Azam itapambana na Chipukizi.
Jumla ya mechi 25 zinatarajiwa kuchezwa katika michuano hiyo ambapo moja pekee itapigwa Uwanja wa Gombani, hii itakuwa ni ile ya nusu fainali ya kwanza, lakini zingine 24 zilizobaki, zitachezwa Uwanja wa Amaan.
Timu shiriki katika michuano hiyo ni; Azam (Tanzania Bara), URA (Uganda), Chipukizi United (Zanzibar), Mlandege (Zanzibar), Simba (Tanzania Bara), Jamhuri (Zanzibar), APR (Rwanda), Singida Fountain Gate (Tanzania Bara), Yanga (Tanzania Bara), Bandari (Kenya), KVZ (Zanzibar) na Vital’O (Burundi).
MAKUNDI
KUNDI A: Azam, URA, Chipukizi United na Mlandege
KUNDI B: Simba, Jamhuri, APR na Singida Fountain Gate
KUNDI C: Yanga, Bandari, KVZ na Vital’O
VIWANJA VITAKAVYOTUMIKA
Amaan (Unguja)
Gombani (Pemba)
RATIBA
DESEMBA 28, 2023
Mlandege vs URA
Chipukizi vs Azam
DESEMBA 29, 2023
Vital’O vs Bandari
Jamhuri vs Singida
DESEMBA 30, 2023
URA vs Chipukizi
Azam vs Mlandege
DESEMBA 31, 2023
Vital’O vs KVZ
Yanga vs Bandari
JANUARI 1, 2024
Singida vs APR
Jamhuri vs Simba
JANUARI 2, 2024
URA vs Azam
KVZ vs Yanga
JANUARI 3, 2024
APR vs Jamhuri
Simba vs Singida
JANUARI 4, 2024
Mlandege vs Chipukizi
Yanga vs Vital’O
JANUARI 5, 2024
KVZ vs Bandari
Simba vs APR
JANUARI 7, 2024
Robo fainali ya kwanza
Robo fainali ya pili
JANUARI 8, 2024
Robo fainali ya tatu
Robo fainali ya nne
JANUARI 10, 2024
Nusu fainali ya kwanza
Nusu fainali ya pili
JANUARI 13, 2024
Fainali
MWANDISHI WETU