The House of Favourite Newspapers

Mapishi ya Shilole Yawateka Wabunge

0

MSANII wa Bongofleva na mjasiriamali katika fani ya mapishi, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amezidi kutusua baada ya kuwateka wabunge kwa mapishi mwanana yaliyowafanya wamfagilie vya kutosha malkia huyo kutoka Unyamwezini.

 

Hayo yameshuhudiwa mwishoni mwa wiki baada ya Shilole kufungua kiota kingine cha masuala ya mahanjumati katika jijini jipya la Dodoma na kuwaalika wabunge, mawaziri na vigogo mbalimbali katika ufunguzi wa mgahawa huo.

 

Aidha, mapokezi aliyoyapata Shilole tangu alipotinga mkoani humo kuandaa mazingira, ikiwamo ndani ya Bunge la Jamhuri yamewaacha mashabiki zake hoi kiasi cha kuamini kuwa ni dhahiri kuwa mwanadada huyo mwenye umbo matata kuwa amefanikiwa kuwateka wabunge.

 

Mbali na utambulisho wa kipekee ndani ya Bunge ambayo umempa sifa na heshima, pia ujio wa wabunge hao katika mghahama wake na sifa walizompatia zimedaiwa kuzidi kumjenga.

 

Achana na mastaa waliompa hongera, pia badhi ya wabunge hao wakiwamo mawaziri, Ummy Mwalimu – Tamisemi, Innocent Bashungwa- Habari, viongozi walioelezea utamu wa mapishi ya Shilole.

Bashingwa kwa upande wake alitoa wito kwa wageni wote wanaotembelea mkoa wa Dodoma kufika katika mghahawa wa Shilole na kujipatia masaptasapta, vivyo hivyo kwa upande wake Ummy Mwalimu ambaye muda wote alionekana kujawa na furaha alimuahidi kumpa sapoti Shilole ili afikie lengo la kuwa na Shishi food International yaani kupasua kimataifa.

 

Hata hivyo, Shishi naye hakubaki nyuma katika kutoa shukrani zake ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika hivi; . (“. “Haijawahi kuwa rahisi sitarajii pia kwamba kuna siku itakuwa rahisi… ni kwa neema za Mwenyezi Mungu. Namshukuru Muumba wangu kwa rehma hii ya kuweza kuungwa mkono na watu wake ninapofanya mambo yangu.

“Nimejawa na furaha na shukrani isiyo kifani, ni heshima ya kipekee sana wamenipa viongozi wangu hawa. Nautafakari ukuu wa Mungu wangu kuweza kuniketisha na wakuu, sina cha kulipa. Asanyeni sana viongozi wangu.”

STORI; MWANDISHI WETU


Leave A Reply