The House of Favourite Newspapers

BABU WA MIAKA 79 ALIYEKUWA DARASA LA KWANZA AKACHA SHULE

 

NDOTO ya elimu ya Mzee Nyamohanga Suguta mwenye umri wa Miaka 79 ambaye mwaka jana alianza masomo ya darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Makerero wilayani Tarime Mkoani Mara imeshindwa kufanikiwa baada ya Mzee huyo kuacha shule akisema haelewi masomo yake.

 

Kwa mujibu wa Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya Tarime amesema kuwa, Mzee Suguta hakusatahili kusoma darasa moja na wanafunzi aliyokuwa nao ambao ni watoto.

 

 

Akizungumza, Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Kennedy Wayoga amesema;

“Mzee Suguta alianza kukacha masomo baada ya kutengwa na wanafunzi wenzake, mwanzoni alikuwa anafurahia kusoma nao kwani walikuwa wanamsaidia kujifunza vitu ambavyo havifahamu ama hajaelewa darasani, hivyo alitengwa ili awe anakuja jioni baada ya muda wa masomo ya kawaida, kuanzia pale akakacha.

“Kusoma alikuwa hajajua vizuri, lakini kuandika na kuhesabu alikuwa ameshajua vyema kabisa,” alisema Mwalimu Kennedy.

 

Msikie Mzee Suguta;

“Kwa kweli naona kichwa changu kimekuwa kizito, kila nikiandika naona nashindwa. Hata mwalimu akinielekeza, nikitoka kidogo nikija kurudi nasahau tena.”

Comments are closed.