The House of Favourite Newspapers

Maradona Kutoa Dola Mil 10 Atakayefanikisha Kumnasa Aliyemzushia Kifo

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona ametangaza ofa ya dola 10,ooo za Marekani (sawa na Tsh. Milioni 22,75) kwa mtu atakayefanikisha kumpata aliyesambaza taarifa kuwa amekufa.

 

Kuenea kwa taarifa za uzushi wa kifo chake kwenye mitandao na vyombo vya habari kumekuja muda mchache baada ya mchezo kati ya Argentina na Nigeria Juni 26 ambapo Argentina ilinusurika kuondoshwa katika hatua ya makundi na timu ya Nigeria.

 

Katika Mchezo uliokuwa wa ushindani mkubwa, Argentina ilipata goli la ushindi dakika za mwisho wa mchezo ikijikusanyia alama 3 kwa kupata magoli 2-0 dhidi ya Nigeria.

 

Maradana amecheza kombe la dunia mara nne akisaidia timu yake kuchukua kombe hilo mwaka 1986, na baadae kuwa mkufunzi wa Argentina kwa miaka miwili.

Comments are closed.