The House of Favourite Newspapers

Fellaini Asaini Kandarasi Kubaki Manchester United, Hadi 2020

KIUNGO wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Ubelgiji, Marouane Fellaini amesaini mkataba wa kuitumikia klabu yake hiyo hadi Juni mwaka 2020, lakini ndani ya mkataba wake kuna kipengele kinachomruhusu kuongeza mkataba wake kabla haujamalizika.

 

Fellaini ambaye kwa sasa yupo na timu yake ya Taifa ya Ubelgiji kwenye michuano ya Fainali za Kombe la Dunia huko nchini Urusi, amesema ataendelea kuitumikia Man U.

“Napenda kuwataarifu kuwa nitaendelea kuwa mchezaji wa Manchester United kwani nimefanya maamuzi haya kwa sababu najisikia furaha kuendelea kuwa hapa. Najiskia kuwa miongoni mwa hii timu hasa chini ya uongozi wa Jose, bado tuna mengi tunayohitaji kuyafikia. Napenda kukushukuru Jose kwa mapenzi yako, unayoonyesha kwangu,” amesema Fellaini.

Meneja wa United, Jose Mourinho raia wa Mreno amesema kuwa anajiskia furaha baada ya kuona Marouane anaendelea kusalia kwa kuwa anaamini siku zote vile anavyotamani kuendelea kuwepo ndani ya klabu.

 

Comments are closed.