MARCELO ALIYESAJILIWA SINGIDA UNITED, ATUA YANGA


Mlinzi wa kushoto, Muharami Issa Said amejiunga na Mabingwa wa Kihistoria wa Tanzania Bara Yanga SC kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Malindi FC ya Zanzibar.

Muharami amekabidhiwa jezi namba 2 ambayo ilikuwa ikitumiwa na beki wa nafasi hiyo Gadiel Michael ambaye amekuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka Jangwani.

Yanga inaweka wazi dili hili ikiwa ni takriban siku sita tangu Juni 30, 2019 Singida United ilipotangaza kumsajili kwa mkataba wa miaka mitatu beki huyu mahiri aliyewika zaidi wakati wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar Januari 2019.

Loading...

Toa comment