The House of Favourite Newspapers

Marekani: Nancy Pelosi Ajiuzulu Kama Kiongozi wa chama cha Democrats katika Bunge

0
Nancy Pelosi.

 

Nancy Pelosi, ambaye ameongoza chama cha Democrats katika Baraza la Wawakilishi la Marekani (Congress) kwa takriban miongo miwili, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo.

 

Pelosi mwenye umri wa miaka 82 ndiye mwanachama wa democrats mwenye nguvu zaidi katika Congress na mwanamke wa kwanza kuhudumu kama spika wa Bunge.

 

Ataendelea kuwakilisha jimbo lake ya California katika baraza la chini la Congress. Haya yanajiri huku Warepublican wakitarajiwa kutwaa tena udhibiti wa Bunge kufuatia uchaguzi wa katikati ya muhula.

Kevin McCarthy wa Republican ameshinda uteuzi wa chama hicho kuwa spika katika Bunge jipya la Congress na huenda akamrithi Bi Pelosi.

 

“Singewahi kufikiria kwamba siku moja ningetoka kwa mama wa nyumbani hadi kuwa spika wa Bunge,” Bi Pelosi alisema katika taarifa yake katika chumba hicho siku ya Alhamisi.

 

“Sitaomba kuchaguliwa tena kuwa uongozi wa Kidemokrasia katika Bunge lijalo. Saa imefika kwa kizazi kipya kuongoza chama cha Democrats,” alisema.

Bi Pelosi atahudumu kama spika hadi Januari wakati Bunge jipya litakapochukua mamlaka, na atasalia katika kiti alichochukua kwa mara ya kwanza mnamo 1987 hadi Januari 2025.

 

Mbunge wa New York Hakeem Jeffries anatarajiwa kwa kiasi kikubwa kuchukua wadhifa wa juu wa uongozi wa chama cha Democrats katika Bunge hilo, jambo ambalo litamfanya kuwa kiongozi wa kwanza wa bunge mweusi katika historia ya Marekani.

 

Spika wa Bunge ni kazi moja ya bunge iliyoainishwa katika Katiba ya Marekani. Baada ya makamu wa rais, inafuatia kwenye mstari wa urais.

Spika na manaibu na wenyeviti wa kamati huamua ni miswada gani inazingatiwa na kupigiwa kura.

 

Wanaweka ajenda na kuamua sheria zinazoongoza mjadala. Bi Pelosi alikua kiongozi wa wachache, cheo kilichoshikiliwa na kiongozi wa upinzani katika Bunge hilo, mwaka wa 2003. Baadaye Democrats walichukua udhibiti wa Bunge hilo kwa mara ya kwanza katika zaidi ya muongo mmoja mwaka wa 2006, na akawa mwanamke wa kwanza kuongoza.

Leave A Reply