The House of Favourite Newspapers

MAREKANI: Siku 10 Baada ya Kuteuliwa, Msemaji wa Ikulu Atumbuliwa

0
Anthony Scaramucci.

Mkuu mpya wa Utumishi wa Rais Donald Trump, John Kelly, aliyeapishwa jana Jumatatu, amemfuta kazi Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu ya Marekani ‘White House’, Anthony Scaramucci ikiwa ni takribani siku kumi tangu alipotuliwa katika wadhifa huo.

 

Siku chache zilizopita, aliyekuwa Mkuu wa Utumishi wa Umma wa Trump, Reince Priebus na msemaji wake Sean Spicer wote walijiuzulu kutokana na uteuzi wa Scaramucci.

 

Taarifa fupi kutoka White House imesema: “Anthony Scaramucci atauacha wadhifa wake kama Mkurugenzi wa Mawasiliano wa White House.

“Bw Scaramucci aliona ni vyema kumpa Mkuu wa utumishi wa Umma John Kelly mwanzo mpya na uwezo wa kuunda timu yake. Tunamtakia kila la heri.”

 

Saa chache kabla, Trump aliandika kwenye Twitter kuhusu takwimu za nafasi za kazi na ajira, na akasisitiza kwamba hakukuwa na mzozo wowote White House wakati huo, Scaramucci alikuwa akijigamba kwamba huwa anaripoti moja kwa moja kwa rais badala ya kupitia kwa Mkuu wa Utumishi wa Umma.

 

Reince Priebus alijiuzulu Ijumaa baada ya Scaramucci kuandika ujumbe kwenye Twitter na kisha kuufuta, ambapo wengi waliuelewa kama tuhuma na tishio dhidi ya yake. Alimpigia pia simu mwanahabari na kumtusi Priebus akisema ni mtu mwenye wasiwasi mwingi na pia akamtuhumu kwa kuvujisha siri kwa wanahabari, huku akimsema vibaya Mwanamikakati Mkuu wa Trump, Steve Bannon.

Leave A Reply