The House of Favourite Newspapers

Poland Yatangaza Kuipa Ukraine Ndege Za Kivita, Marekani Yakataa

0

Serikali ya Poland imetangaza kuipa msaada Ukraine wa ndege za kisasa za kivita, MiG-29 ili kukabiliana na mashambulizi ya anga kutoka kwa majesi ya Urusi lakini Marekani imekataa uamuzi huo na kueleza kwamba unaweza kuhatarisha zaidi usalama.

Poland ilieleza kwamba itazipeleka ndege hizo Marekani kisha taifa hilo ndiyo lizifikishe Ukraine ili kukwepa kuvunja kanuni za Umoja wa Kujihami wa Nato lakini Marekani imelikataa suala hilo.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon imesema hatua hiyo inahitaji mjadala mpana kwa sababu inaweza kuyaingiza matatizoni mataifa yote wanachama wa Nato na kwamba mpango wa kupeleka ndege hizo Ukraine hauwezekani.

Akizungumza usiku wa jana, Machi 9, 2022, Katibu Mkuu wa Pentagon, John F. Kirby amesema Marekani imeshtushwa na taarifa iliyotolewa na serikali ya Poland kwamba tayari imekabidhi ndege hizo za kivita kwa Marekani kwa ajili ya kuzipeleka Ukraine na kueleza kwamba mazungumzo ya karibu yanaendelea.
“Tunaendelea kuwasiliana kwa ukaribu na mataifa yote rafiki, uamuzi wa Poland unaonesha ni kwa kiasi gani suala hili ni gumu,” alisema Kirby.

Siku kadhaa zilizopita, Rais wa Ukraine, Volodomyr Zelensky, aliomba msaada wa kulifunga anga la Ukraine na kupatiwa ndege za kivita ili kupambana na mashambulizi ya majeshi ya Urusi ambayo kwa asilimia kubwa yamekuwa yakitokea angani.

Uamuzi huo wa Marekani kukataa kushirikiana na Poland kuzifikisha ndege hizo Ukraine, unaweza kuwa pigo kubwa kwa Ukraine katika kipindi hiki ambacho inahitaji sana msaada wa ndege za kivita.

Inaelezwa kwamba Poland ambayo nayo I mwanachama wa Umoja wa Kujihami wa Nato, imechukua uamuzi wa kutangaza hadharani kutoa ndege hizo na kuzikabidhi kwa Marekani ili zipelekwe Ukraine, baada ya kutorodhishwa na namna Marekani na Nato wanavyolifanyia kazi suala la kwenda kuisaidia Ukraine kupambana na Urusi.

Msafara wa mabasi ya kuwahamisha raia kutoka mji wa Mariupol siku ya Jumanne (Machi 8, 2022).
Mwanajeshi wa Ukraine katika mji wa Sumy.

 

Leave A Reply