The House of Favourite Newspapers

Marekani Yatishia Kuiwekea Vikwazo ICC

0

SERIKALI ya Marekani imetishia vikwazo dhidi ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC ikiwa itaendelea na mikakati yake ya kuwashtaki raia wa Marekani.

 

Mahakama hiyo kwa sasa inatathmini kuwafungulia mashtaka wanajeshi wa Marekani kwa madai ya kuwatesa wafungwa nchini Afghanistan.

 

Mshauri wa masuala ya usalama ya kitaifa John Bolton alisema mahakama hiyo sio halali na kuapa kuwa Marekani itafanya kila iwezalo kuwalinda raia wake.

 

Mwezi Oktoba mwaka 2016, Burundi na Afrika Kusini waliandika kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuelezea uamuzi wao wa kuondoka kutoka ICC.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta  alikabiliwa na kesi katika mahakama hiyo aliserma makahama hiyo ni chombo ya siasa za dunia lakina sio kuhusu haki ilizotakiwa kutoa.

 

Kutodhika na mahakama hiyo kumetokana na hisia kuwa ICC ilikuwa inawalenga waafrika na haiheshimu siasa na uhuru wa nchi za Afrika,kesi kumi kati ya tisa zilizo, kwenye mahakama hiyo zinahusu nchi za Afrika.

 

Mahakama hiyo inachunguza na kuwaleta hukumuni wale wanaohusika kwenye uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, ikiingilia kati wakati mahakama za nchi ambazo haziwezi kuwahukumu.

Leave A Reply