The House of Favourite Newspapers

Mariam Biriani azua balaa ukumbini – Video

WAKATI skendo ya picha chafu ikiwa bado haijapoa, mjasiriamali aliyejizolea umaarufu Bongo kwa mapishi ya biriani, Mariam Selemani a.k.a Mariam Biriani, ameibua balaa ukumbini baada ya midume yenye uchu kumkodolea macho wakati akikatiza ukumbini kuelekea jukwaani.

 

Ilikuwa juzi Ijumaa ndani ya kiwanja cha Forty Forty Lounge kilichopo Tabata-Bima, jijini Dar es Salaam, ambapo Bendi ya Mapacha Orijino chini ya Khalid Chokoraa ilikuwa ikikamua.

Wakati bendi hiyo ikiendelea kufanya yake jukwaani, mwanadada huyo aliitwa apande mbele, ndipo akaanza kutembea kwa maringo akiwa amevalia kigauni chake kifupi cha rangi ya bluu ya kupauka.

 

SHANGWE KAMA LOTE

Ilikuwa ni kama staa fulani mkubwa ametokea ghafla wakati alipokuwa akitembea kwa maringo huku akirusha ‘mawe’, jambo lililozusha shangwe kwa midume waliokuwa ukumbini humo.

Balaa lilikuwa kubwa zaidi baada ya mrembo huyo mwenye umbo la kuvutia alipokuwa akisaidiwa kupanda jukwaani ambapo midume mikware ilianza kumpigia makofi kwenye umbo lake lililojazia.

Wakati mdada huyo akiwa jukwaani hapo midume kadhaa ilionekana kushika vichwa kuonesha kuchanganyikiwa na umbile la mdada huyo huku wengine wakimtunza kabla hajaanza kufanya chochote.

“Huyu dada jamani ameumbika jamani, ana haki ya kushangiliwa na kila mtu. Yaani ni balaa kabisa aisee,” alisikika akisema jamaa mmoja aliyekuwa ukumbini hapo.

ATOA NENO

Akiwa jukwaani Mariam Biriani aliwaambia wapenzi wa biriani kuwa kwa kipindi hiki amesitisha kutoa huduma hiyo lakini baada ya kuisha mwezi huu anatarajia kuwafanyia sapraiz ya nguvu wateja wake.

“Nimesitisha kwa muda biashara kwa heshima ya mwezi huu, ukiisha mambo yatakuwa kama kawa, naw aahidi surprise ya nguvu mkija ofisini kwangu,” alisema Mariam Birian.

MIDUME YAMSARANDIA

Hata Mariam Birian alipomaliza kutoa neno na kushuka chini, watu waliendelea kumshangilia, huku midume mikware ikianza kumfuatilia nyuma mpaka alipokwenda kukaa.

Mwanahabari wetu alizungumza na Mariam Biriani ukumbini hapo kuhusiana na midume mikware iliyokuwa ikimfuata nyuma na kumshangilia, akasema: “Hakuna cha ajabu. Ni kawaida.”

 

“Haya ndiyo maisha yangu, mara nyingi nikipita huwa nashangiliwa kama hivi, ndiyo maana nasema hakuna cha ajabu. Nimeshazoea sasa,” aliongeza Mariam Biriani.

STORI: RICHARD BUKOS, DAR

Comments are closed.