The House of Favourite Newspapers

Siri Nzito ya Bwana Mpya wa Zari, Utashangaa!

DAR ES SALAAM: MREMBO wa Kiganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ anaendelea kutikisa vyombo vya habari, safari hii zengwe limeibuka kumhusu bwana halali anayemmliki mrembo huyo kwa sasa, Ijumaa Wikienda limesheheni ubuyu kamili.

 

Mitandao mbalimbali ya habari za mastaa nchini Uganda anakotokea mrembo huyo imeeleza kuwa, kuna usiri mzito ambao Zari mwenyewe anao kuhusu mwanaume ambaye anatoka naye kimapenzi kwa sasa.

 

Mitandao hiyo imeeleza kuwa, kutokana na wanaume tofauti ambao picha zao zimekuwa zikivuja, ni dhahiri Zari atakuwa anawayumbisha akili mashabiki wake kwani haileweki ni nani hasa ambaye kweli ni mpenzi wake.

 

WANAUME WENYEWE…

Licha ya watu wengi kuwachanganya mitandaoni wakidhani ni mwanaume mmoja, uchunguzi wa Ijumaa Wikienda ulibaini kuwa, wanaume hao ni tofauti kutokana na kuwa na maumbo na rangi tofauti.

 

Uchunguzi huo uliweza kuwafikia baadhi ya mastaa wa Kibongo ambao wapo karibu na familia ya mpenzi wa zamani wa mrembo huyo Nasibu Nasibu ‘Diamond’ ambao pia walikuwa karibu na mrembo huyo ambao walisema, Zari anacheza na akili za Watanzania.

 

“Amewachezesha sana mashabiki wake, awali ilianza tu jina kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikawa kila mtu ni King Bae…King Bae lakini hakuna aliyekuwa anamjua huyo King Bae mwenyewe anafananaje,” alisema msanii mmoja akiomba hifadhi ya jina na kuongeza:

 

“Baadaye akaweka picha ya yule kaka aliyekuwa amekaa naye kwenye kochi akiwa amemshika kiuno na watu wakaamini kwamba ndiye King Bae mwenyewe aliyekuwa akimzungumzia, mi nakwambia unaweza kuta hata huyo King Bae pia hayupo.”

 

WENGINE WAIBUKA

Baada ya watu wengi kuamini kuwa King Bae ndio huyo ambaye katika picha haonekani sura kwa sababu ya picha hiyo kukatwa na kuonesha mwili mzima hadi kuishia kwenye mdomo, picha nyingine ziliibuliwa ambapo Zari alionekana akiwa na wanaume tofauti.

 

Kuna ambayo Zari alionekana yupo katika mandhari ya kijijini, akiwa amekaa kwenye kigoda na jirani yake akiwepo mwanaume huyo ambaye amezibwa usoni kwa alama ya kopa. Kwa upande wake mwanaume huyo aliyeonekana ana umbo dogo (tofauti na yule wa kwenye kochi), alikuwa amevaa koti la bluu na fulana ndani.

 

Wadau mbalimbali walishindwa kumuelewa mwanaume huyo kama ndiye King Bae au la, wakabaki tu kumpongeza kwa kuinjoi maisha na mwanaume wake huyo huku wengi wakimponda kwa kumhoji kwa nini amzibe kama kweli ni mali yake.

 

Kama hiyo haitoshi, kuna mwingine ambaye alionekana naye akiwa amevaa koti kali lakini naye amezibwa kichwa kizima na alama maarufu za kwenye simu za kisasa (emoji) ya mtu anayelia machozi.

 

MWINGINE NA SINGLENDI

Aidha, pia kuna mwingine alikuwa amevaa singlendi nyeupe ambaye kwa mujibu ya maoni mbalimbali yaliyowekwa mtandaoni, walisema mwanaume huyo hafanani na Zari kutokana na muonekano wake tofauti na wanaume wengine.

 

NI KICHECHE?

Baadhi ya wachangiaji kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii walidai kwamba mrembo huyo amekuwa na mahusiano na wanaume wengi kwa sasa (kicheche) kwani haiwezekani picha hizo zinazomuonesha akiwa na wanaume tofauti zivuje halafu asikanushe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kama ambavyo amekuwa akifanya katika baadhi ya mambo.

 

MWINGINE AFANANISHWA NA YULE WA KOCHI

Kuna mwanaume mwingine ambaye alionekana akiwa katika muonekano wa kuwa ‘mtu na mtuwe’ ambaye alikuwa amevaa suti ya bluu huku kichwani akiwa amezibwa na emoji ya kopa.

 

WOTE NI WAKE?

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, kuna uwezekano mkubwa mrembo huyo akawa ameamua kuwarusha roho mashabiki wake kama ambavyo aliwahi kufanya hivyo kwa kujiachia na magari ya kifahari miaka ya nyuma.

 

“Huyu anacheza tu na akili za Watanzania haswa wale ambao wanaendelea kumfuatilia baada ya Diamond kumuanika mpenzi wake mpya Tanasha Donna hivyo wana hamu ya kutaka kujua naye atamuanika nani kama mpenzi wake.

 

“Anawafanyia bosheni tu kama vile alivyokuwa anabadili magari mengi ya kifahari (tazama picha ukurasa wa mbele) miaka ya nyuma ambayo yalikuwa na jina lake na mpaka sasa hayaonekani tena,” Ijumaa Wikienda lilielezwa katika uchunguzi wake.

 

ZARI MWENYEWE HATAKI KOHOJIWA SANA

Katika mahojiano ambayo mrembo huyo aliyafanya alipokuja Bongo hivi karibuni alipoulizwa kuhusu mwanaume anayetoka naye kwa sasa ni yupi haswa hakutaka kufafanua kwa undani zaidi tu ya kusema anaye mtu na yuko tayari kumzalia.

 

MHARIRI

Maisha ya Zari yameonekana kujaa usiri na ‘usanii’ mwingi hususan katika maisha ya uhusiano na utajiri hivyo kama kweli King Bae yupo na ni miongoni mwa wanaume hao aliowaziba sura na kuibua zengwe la utata wa uwepo wake, basi ni vema Zari akamfungua sura na kuiweka wazi jamii inayomfuatilia vinginevyo ataonekana kama mtu ambaye bado anatapatapa na hajajua ni mwanaume yupi anafaa kuchukua mikoba ya Diamond.

STORI: ERICK EVARIST, DAR

Comments are closed.