Marlaw ataja ukimya wake, hatima yake na Besta

MWANAMUZIKI  Lawrence Marima maarufu kama Marlaw ambaye aliwahi kutamba na wimbo wa ‘Bembeleza’,  leo Septemba 19 2019,  amefika studio za +255 Global Radio zilizopo Jengo la Global Group Sinza Mori jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kutambulisha nyimbo zake mpya za ‘Baraka’ na ‘Taa’ ambazo zimekuja miaka tisa baada ya ukimya wake kwenye muziki.

 

Marlaw (katikati) akiwa na watangazaji wa +255 Global Radio.

Marlaw amepiga stori na watangazaji wa Bongo255 na kufunguka vitu vingi ikiwemo nafasi yake kwenye muziki ambayo anahisi bado ipo kutokana na vitu vizuri alivyoviandaa kwa ajili ya mashabiki wengi wanaomdai kazi mpya kila wanapomuona.

Marlaw anasema sababu kubwa iliyomfanya awe kimya kwa muda mrefu ni kutaka kujiboresha kwa kila kitu ikiwemo ubunifu, ubora, uimara na maisha kwa ujumla.

 

Akifanya mahojiano na Global Radio.

Marlaw amesema licha ya kujiandaa kuja upya kwenye muziki, familia yake na Besta ambayo imebarikiwa watoto watan,  moja ya vitu vilivyomfanya awe kimya kwa miaka mingi.

 

…Akisaini kitabu cha wageni.

Kuhusu mke wake, Marlaw amesema Besta yupo ‘fiti’ na mipango ya kurudi kwenye muziki ipo kwani kazi walizofanya ni nyingi na muda wowote zinaweza kuachiwa.

ZISIKILIZE HAPA CHINI NYIMBO MPYA  ZA MARLAW ‘TAA’ NA ‘BARAKA’

 


Loading...

Toa comment