visa

MARRY MAWIGI SIDANGI, TAMTHILIYA ZINALIPA

Mwigizaji wa filamu Bongo, Mary Mawigi amefunguka kuwa, kwa sasa maisha yake anayaendesha kwa kucheza tamthiliya ikiwa ni baada ya soko la filamu kukataa.

 

Akipiga stori na Amani, Mary alisema maisha yake yanaenda vizuri kuliko hata wakati alipokuwa akitegemea kushirikishwa kwenye filamu hivyo tamthiliya zinalipa zaidi na hategemei kudanga kama watu wengi wanavyodhani kwamba wasanii wa kike wa filamu wanakula kwa mgongo wa wanaume

.

“Siku hizi nimekuwa bize sana na tamthiliya na namshukuru Mungu maisha yanaenda, nakula kwa nguvu zangu mwenyewe, tamthiliya zinalipa sana kuliko filamu,” alisema Mary ambaye anacheza Tamthiliya ya Huba inayorushwa na DSTV.
Toa comment