The House of Favourite Newspapers

Martial, Vardy wachezaji wenye kasi zaidi EPL

0

martial

Anthony Martial (kushoto) aliweka rekodi hiyo wakati Manchester United ilipotoka sare ya 3-3 dhdi ya Newcastle.

Staa wa Klabu ya Manchester United, Anthony Martial na straika wa Leicester, Jamie Vardy wameweka rekodi ya kuwa wachezaji wenye kasi zaidi kwenye Ligi Kuu ya England msimu huu kwa mujibu wa takwimu za wachezaji kutoka EA Sports.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa Vardy alifikia rekodi hiyo baada ya kucheza kwa kasi ya maili 22 kwa saa (22mph) ndani ya sekunde tano alipoisaidia Leicester kuichapa West Ham 2-1, mwezi Agosti mwaka jana.

Jamie

Straika wa Leicester, Jamie Vardy (kushoto) yeye aliweka rekodi wakati timu yake ipoichapa West Ham 2-1 Agosti mwaka jana.

Anthony Martial naye alifungana na Vardy kwa kukimbia kwa spidi ya maili 22 kwa saa (22mph) wakati Manchester ikitoka sare ya 3-3 dhidi ya Newcastle.

Beki wa Leicester, Jeffrey Schlupp yeye anashika nafasi ya tatu kwa spidi ya maili 21.9 kwa saa (21.9mph) huku mchezaji wa Tottenham, Kyle Walker akishika nafasi ya nne akiwa na spidi ya maili 21.8 kwa saa (21.8mph).

Leave A Reply