MARY MAWIGI, IRENE PAUL WACHAPANA LOKESHENI

Irene Paul

STAA wa filamu za Ki­bongo, Mary Mawigi na mwenzake Irene Paul hivi karibuni walidaiwa kupigana lokesheni walipokuwa wakirekodi mwendelezo wa Mchezo wa Huba unaoendelea kwenye televisheni ya DSTV.Sosi aliyekuwa eneo la tukio alilitonya Ijumaa Wikienda kuwa, chanzo cha ugomvi wa wawili hao ni baada ya kupis­hana lugha ambapo Irene alim­sukuma Mary ambaye naye alimjibu kwa kumpiga makofi na ndipo ugomvi ulipozuka.

Ijumaa wikienda lilimsaka Mary ili kuongelea madai haya na alipopatikana alisema kuwa asingependa kuongelea masu­ala ya lokesheni kwani yalipita na sasa hana ugomvi wowote na Irene.

“Jamani nani aliyewaambia mambo hayo, binadamu huto­fautiana na kumaliza matatizo yao, mimi na Irene tupo sawa sasa, nisingependa kuyaonge­lea zaidi,” alisema Mary. Irene naye aliposakwa kuongelea ugomvi huo simu yake iliita bila kupokelewa, alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno aliusoma lakini hakujibu.

STORI: Hamida Hassan, Ijumaa Wikienda

Loading...

Toa comment