The House of Favourite Newspapers

MASANJA: KANYE WEST ACHA KUVUTA BANGI

Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’

 UNAWEZA kujiuliza inawezekana kweli msanii wa vichekesho ambaye pia ni mchungaji, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ameweza ‘kumfyatukia’ rapa kutoka Marekani, Kanye West kwa kumwambia aache bangi?

Kama ulikuwa hujui, jua sasa; hii imetokea juzi tu katika ukurasa wa kijamii wa Twitter wa Kanye West ambapo rapa huyu aliandika maneno matatu tu; ‘We are Gods’ akimaanisha, ‘Sisi ni Miungu’ ndipo povu kubwa likaanza kumtoka Masanja kwa kumjibu kwa Kiswahili (sijui sasa kama ujumbe ulikuwa unamfikia).

Masanja aliandika meseji hizi za kumjibu Kanye West; “Huwaga una umama sana.”“Acha kuvuta bangi.”“Wewe ni kenge.”

STAR SHOWBIZ

Comments are closed.