Kartra

Masau Bwire: Tutawakung’uta Simba Tena

OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, amesema kuwa watawakung’uta tena wapinzani wao, Simba watakapokutana katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili.

 

Katika mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru, Ruvu Shooting ilishinda bao 1-0 ilikuwa ni zama za Sven Vandenbroeck ambaye alibwaga manyanga na sasa yupo Kocha Mkuu, Didier Gomes.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi,Bwire alisema kuwa wanajua kwamba wapinzani wao wanafikiria kulipa kisasi ila wasahau suala hilo.

 

“Tunajua kwamba Simba wanafikiria kulipa kisasi, hilo wasahau kwani sisi tupo tayari kuwapapasa, kuwatingisha na kuwakung’uta kwa mara nyingine tena na kujidhihirisha sisi ni zaidi,” alisema Bwire.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Juni 3, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam


Toa comment