The House of Favourite Newspapers

Mashabiki 8 Wafariki Uwanja wa Soka Senegal

0
Ramani ya Senegal.

Watu wanane wamefariki dunia baada ya kukanyagana walipokuwa wakishuhudia michuano ya ligi ya soka nchini Senegal.

Waziri wa Michezo wa Senegal, Matar Ba, amesema msichana mdogo ni miongoni mwa waliopoteza maisha  na majeruhi 60 wamefikishwa hospitali mjini Dakar.

Nyavu za moja ya magoli uwanjani zikiwa zimechanika baada ya vurumai hiyo.

Habari zinasema mashabiki wa timu mbili za mpira wa miguu zilizokuwa zinacheza walianzisha vurugu hiyo kwa kushambuliana baada ya mchuano uliochezewa katika uwanja wa michezo wa Demba Diop Stadium kumalizika.

Katika vurumai hiyo, sehemu ya ukuta wauwanja huo  iliporomoka wakati  idadi kubwa ya watu walipokuwa wakisukuma kuondoka uwanjani hapo. Serikali imeahidi  kuchukua hatua madhubuti ili kuzuia matukio  kama hayo kutokea tena nchini Senegal.

Ratiba ya Mazishi ya Mke wa Waziri Mwakyembe Yatolewa, Itazame Hapa

Leave A Reply