The House of Favourite Newspapers

Mashabiki wa Mchiriku na Taarab karibuni Pasaka Dar Live

0

msagasumu2

Msaga Sumu akizidi kuwachizisha mashabiki wake Dar Live.

Mashabiki wa Muziki wa Mchiriku na Taarab wanatarajiwa kushuhudia historia itakayo andikwa na wakali wa muziki huo, Machi 27, mwaka huu (Sikukuu ya Pasaka) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Muziki huo wa Mchiriku ambao kwa jina jingine unatambulika kama Singeli umekuwa ukiwateka vijana wengi huku ukichezwa kwa staili ya kipekee.
Akizungumza na Over The Weekend, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa kwa mara ya kwanza Mchiriku utawakusanya wakali wote wanaouimba na kuwasha moto ndani ya Dar Live.

ALIKIBA1

Mashabiki wakiendelea na burudani Dar Live.

“Haijawahi kutokea lakini kwa mara ya kwanza, Dar Live itawashusha wakali wote wa Mchiriku wanaobamba Bongo ambao ni Msaga Sumu, Dogo Mfaume, Siza na Segere, Jagwa, Sholo Mwamba pamoja na Man Fongo.
“Ili kunogesha muziki huo, mashabiki pia watapata fursa ya kuzishuhudia bendi kali za Muziki wa Taarab, Ogopa Kopa iliyo chini ya Khadija Kopa pamoja na East African Melody,” alisema Mbizo.

msagasumu4
Mbizo aliongeza kuwa siku hiyo pazia la burudani litafunguliwa mapema kuanzia saa mbili za asubuhi ambapo kutakuwa na burudani kwa watoto wote, watacheza michezo mingi ikiwa sambamba na mazingaombwe, sarakasi, kuogelea na kubembea kwa kiingilio cha shilingi 2,000 tu.
“Burudani ya kibabe itaanza saa mbili za usiku ambapo mashabiki wote wa Mchiriku na Taarab watajimwayamwaya kwa kupata shoo ya nguvu kutoka kwa wakali hao ambapo watapata bahati ya kupiga picha (red carpet) na mastaa hao sambamba na kuimba na kucheza nao stejini kwa kiingilio cha shilingi 6,000 tu,” alisema.

Leave A Reply