The House of Favourite Newspapers

NMB, Fastjet kuwawezesha wateja kununua tiketi kwa urahisi

0

Agreement pic

Kaimu Afisa Mkuu wa wateja wadogo na kati NMB (kulia)- Bw. Abdulmajid Nsekela akifurahia pamoja na Mtendaji Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker na Meneja Mkuu wa FastJet Bw. John Corse baada ya kukamilisha hafla ya makubaliano hayo iliyofanyika katika hoteli ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.

Ineke signing agreement

Mtendaji Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker na Meneja Mkuu wa Fastjet nchini Bw. John Corse wakieka saini mkataba ambao utawanufaisha wateja wa NMB na ambao sio wateja wa NMB kuweza kulipia tiketi za usafiri wa ndege kupitia NMB Mobile na matawi ya benki yaliyopo nchi nzima.

Nsekela

Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na Kati wa NMB – Bw. Abdulmajid Nsekela akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jinsi gani wateja wa NMB na ambao sio wateja wanaweza kununua tiketi kwa kupitia NMB mobile na matawi ya NMB.

Sasa wateja wa NMB na wasio wateja wa NMB wanaweza kufanya malipo ya tiketi za kusafiria za Fastjet kupitia matawi ya NMB yaliyopo nchi nzima au kwa kupitia NMB Mobile. Njia hizi za malipo zitawarahisishia wateja zaidi ya milioni mbili wa benki ya NMB na zaidi ya wateja laki mbili wa kampuni ya ndege ya Fastjet kununua tiketi zao za kusafiria kwa urahisi zaidi. Kwa wale wateja wa NMB, wanaweza kukamilisha manunuzi ya tiketi kwa kutumia NMB mobile au kupitia zaidi ya matawi 170 ya NMB yaliyopo nchi nzima.

Akiongea na waandishi wa habari, Mtendaji Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker alisema,”Tunayo furaha kushirikiana na fastjet ambayo ni kampuni kubwa ya ndege na yenye gharama nafuu nchini hivyo tunaamini kwamba ushirikiano huu utasaidia kuleta huduma zetu karibu zaidi na watu kupitia mtandao na matawi yetu nchini”.

Kulipia tiketi ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kufanya maandalizi y safari kupitia tovuti ya fastjet au vituo vyao vya mauzo ambapo utapata namba ya kumbukumbu yenye tarakimu nane. Ukishapata hii namba ya kumbukumbu, kwa wateja wa NMB unaweza kulipia kwa kupitia NMB mobile Piga *150*66# kisha chagua Malipo ya Bili halafu chagua Fastjet.

Kwa wateja wasio wa NMB, wanaweza kutembelea tawi lolote la NMB ili kufanya malipo. Ukishafanya malipo, utapata SMS ya uthibitisho wa malipo pamoja na ticket itakayotumwa kwenye barua pepe ambayo utakua umeisajili wakati wa kupanga safari. Hakikisha una namba yako ya kumbukumbu wakati wote ili ikuwezeshe kufanya malipo popote ulipo.

Leave A Reply