The House of Favourite Newspapers

Mashabiki wa Simba/Kaizer Chiefs Ya Afrika Kusini Wadaka Tiketi za Bure

0
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, Songolo Bilaly (kulia) akimkabidhi tiketi.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers,(kushoto) Juma Johanes akimkabidhi tiketi msomaji wa Gazeti la Championi.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, Songolo Bilaly (katikati) akipozi katika picha ya pamoja na wadau wa gazeti la Championi mara baada ya kukabidhi tiketi.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers,(kulia) Juma Johanes akimkabidhi tiketi msomaji wa Gazeti la Championi.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers,(kulia) Juma Johanes akimkabidhi tiketi msomaji wa Gazeti la Championi.
Msomaji wa Championi akionesha tiketi yake.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers,(wa pili kushoto) akipozi na wasomaji wa Gazeti la Championi.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers,(wa pili katikati) akipozi na wasomaji wa Gazeti la Championi.

 

Msomaji wa Championi akionesha tiketi yake.

 

KAMPUNI ya Global Group kupitia gazeti namba moja la michezo Tanzania, Championi limetoa zawadi za tiketi kwa wateja wake ili waweze kushuhudia mtanange wa leo kati ya Simba na Kaizer Chiefs Ya Afrika Kusini.

 

Anthon Adam, Mkuu wa Kitengo cha Usambazaji kutoka Global Group amesema kuwa ni kawaida ya kampuni hiyo kurudisha fadhila kwa wasomaji wake kwa kuwapa tiketi hizo ikiwa ni pamoja na zawadi mbalimbali ambazo kampuni hiyo imekuwa ikizitoa.

 

“Hii ni kwa kawaida yetu kurudisha fadhila kwa wasomaji wetu kwani wamekuwa wakituunga mkono, hivyo ni jambo jema kuwarudishia kile tunachokipata kutoka kwao, kwa kuwa sote ni familia ya Championi. Amesema.

 

“Wasomaji wetu tuliowakuta wakiwa na nakala ya gazeti la Championi leo Jumamosi  Mei 22, 2021 tumewapa tiketi ya kwenye mechi ya Simba dhidi ya Kaizer Chiefs Ya Afrika Kusini. hii imekuwa ni desturi yetu kuwapa tiketi wasomaji wetu wanaokutwa wakiwa na nakala ya gazeti,” aliongeza.

Leave A Reply