The House of Favourite Newspapers

MASHABIKI WA SIMBA WATEKA UWANJA WA SINGIDA

Mashabiki wa klabu ya Simba wakishangilia kabla ya mechi ya leo dhidi ya Singida United katika Uwanja wa Namfua.
Wapenzi wa Simba wakielekea kwenye nafasi zao kabla ya kuanza kwa mpambano.
Mwonekano nje ya uwanja ambapo majezi ya klabu mbalimbali, yakiwamo ya Simba na Yanga yakiuzwa kwa mashabiki.

Mashabiki wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa Namfua kuishangilia timu yao itakayocheza dhidi ya Singida United jioni ya leo.  Mashabiki hao wameipongeza timu hiyo ya Simba na viongozi wao kwa kuwapatia furaha inayotokana na klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi ya Vodacom nchini.

 

Pamoja na kubakiwa na mechi kadhaa kabla ya kumalizika ligi hiyo, Simba tayari imechukua ubingwa huo tangu siku klabu ya Yanga ilipofungwa mabao 2-0 na timu ya Prison ya Mbeya.

 

Kabla ya mchezo wa leo, Simba imebakiwa na michezo mitatu ambapo ina pointi 65 zisizoweza kufikiwa na timu nyingine yoyote.  Inafuatiwa na Azam iliyobakiwa na michezo mitatu na pointi 49 na Yanga ni ya tatu ikiwa na mechi tano mkononi na pointi 48.

(PICHA NA MUSA MATEJA | SINGIDA -GLOBAL PUBLISHERS)

Comments are closed.