The House of Favourite Newspapers

Kenya Yarusha Satelaiti Kutokea Japan (Video + Picha)

Satelaiti hiyo ikiwa angani baada ya kurushwa.

 

KENYA ilirusha satelaiti yake ya kwanza jana kutokea nchini Japan ambako ilishuhudiwa na  wanasayansi mbalimbali wa masuala ya anga za juu kutoka Kenya. Chombo hicho kilirushwa kutokea makao ya Uchunguzi wa Sayansi ya Anga za Juu nchini Japan, (JAXA).

Nchini Kenya kwenyewe raia walifuatilia tukio hilo moja kwa moja kwenye mtandao wa YouTube, na sherehe maalumu ya kulishuhudia iliafanyika katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

Mtaalam akifanya matayarisho ya urushaji wa satelaiti hiyo.

 

Satelaiti hiyo ndogo ni ya thamani ya dola milioni moja – gharama inayoonekana kuwa ndogo kifedha kwa kiwango cha sayansi ya anga za juu.

 

Wahadhiri wa vyuo vikuu wanasema satelaiti hiyo inaweza kutoa huduma tofuati ikiwemo kukusanya taarifa zitakazosaidia katika kilimo na usalama, kutabiri hali ya hewa na hata kukabiliana na majanga.

 

Kenya kwa sasa inakabiliwa na janga la mafuriko ambalo limesababisha maafa makubwa.

Takriban watu mia mbili wamepoteza maisha yao, huku wengine zaidi ya laki mbili wamepoteza makaazi yao.

Comments are closed.