The House of Favourite Newspapers

Mashabiki wataka jina la mtoto wa pili wa Kim Kardashian liwe Easton West

0

2F09542900000578-0-image-a-1_1449331604346 Kim Kardashian.

New York, Marekani

BAADA ya kujifungua mtoto wa kiume jana (Jumamosi), mashabiki wa mwanamitindo na mtangazaji maarufu wa Kipindi cha Keeping Up With The Kardashian, Kim Kardashian wameibuka katika mitandao ya kijamii na kumtaka Kim kumuita mtoto huyo jina la Easton West.

2F0595EA00000578-3347401-image-a-12_1449332127626Kim Kardashian akiwa na mumewe Kanye West.

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Kim Kardashian mashabiki hao walionesha hisia zao ambapo kila mmoja alipendekeza aitwe Easton West.
“Najua ataitwa tu Easton West.”
“Natamani kweli aitwe Easton West.”

Zilisomeka baadhi ya meseji hizo kwenye ukurasa wa Twitter.
TAngu Kim ana ujauzito wa mtoto huyu aliyejifungua jana, hakuwahi kuweka wazi jina la mtoto hali inayoendelea kuzua sintofahamu kwa mashabiki wake baada ya mtoto wake wa kike wa kwanza kumuita North West.

Capture

Leave A Reply