The House of Favourite Newspapers

Mashindano ya Johnnie Walker Waitara Trophy Yahitimishwa jijini Dar

0

VETERANI wa mchezo wa Gofu Dkt. Edmund Mndolwa (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 1,500,000/-mshindi wa kwanza ambaye ni mchezaji wa kulipwa (profesional player)  kutoka Klabu ya Gofu ya Lugalo Bryson Nyenza baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Johnnie Walker Waitara Trophy yaliyodhamini na Kampuni ya Bia ya Serengeti Kupitia kinywaji chake cha Johnnie Walker.

Mshindi wa jumla katika mashindano ya Johnnie Walker Waitara Trophy, Khalid Shemndolwa (wa kwanza kushoto) akikabidhiwa zawadi ya vikombe baada ya kuibuka mshindi. Wa kwanza kulia ni mwakilishi kutoka Resolution Insurance akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Vanance Mabeyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Mnyepe, na Mkuu wa Majeshi wa Malawi, Jenerali Vincent Nundwe.

Wasanii wa kikundi cha ngoma wakitumbuiza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya Johnnie Walker Waitara Golf 2020 yaliyofanyika katika Viwanja vya Gofu vya kijeshi vilivyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kulia) akimkabidhi zawadi ya kinywaji cha Johnnie Walker, Mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika mchezo wa Gofu. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana wakati wa kuhitimisha mashindano ya Johnnie Walker Waitara Trophy 2020.

Leave A Reply