The House of Favourite Newspapers

Mashindano ya Qur-an ya Dunia Yafanyika Diamond Jubilee, Dar (Pichaz +Video)

0

Abdulmjid Mujahid kutoka Yemen ameibuka mshindi wa mashindano ya kimataifa ya Qur-an yaliyozishindanisha nchi kumi ambapo mshindi amezawadiwa dola 5000 za Kimarekani huku Ubalozi wa Kuwait ukimzawadia dola 500, mshindi wa pili wa mashindano hayo ni Omary Abdallah kutoka Tanzania ambaye naye amezawadiwa dola 4000 na dola 300 kutoka Ubalozi wa Kuwait.

Mashindano hayo yameshirikisha nchi kumi zikiwemo Uganda, Mali, Tanzania Bara, Yemen, Russia, Uingereza, Libya, Bangladesh, Marekani na Jumuiya ya Falme za Kiarabu (United Arab Emirates).

Pia Mashindano hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali yakiongozwa na Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy na Mlezi wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi, Muft Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na mgeni rasmi kutoka Saudi Arabia, Abdallah Basfar ambaye ni msomaji Qur-an wa kimataifa.

Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeiry akiongea katika Mashindano ya Qur-an ya Dunia Yafanyika Diamond Jubilee, Dar.

Akihutubia katika mashindano hayo Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Ally Seif Iddy ameeleza kuwa vijana wamekosa adabu na matendo ya ulawiti, mauaji kwa watoto wachanga, unyanyasaji, mauaji ya wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa yakiripotiwa, huku akieleza kuwa ahamini kama Mwenyezi Mungu anayaridhia matendo haya, hivyo tabia za Watanzania na Waislamu ziendane na maamrisho ya Qur-an.

Pia Makamu wa Rais Balozi Seif Ally Iddy ameongeza kuwa bora ni mwenye kujifunza Qur-an na akawafundisha wengine Mwenyezi Mungu amewanasihi Waislamu katika kitabu chake kitukufu.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amewapongeza wanafunzi wa Kiislamu wanaojifunza Qur-an kwani kufanya hivyo ni kuiendea jamii njema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Tanzania, Sheikh Othman Ally Kaporo amewataka wadau wa masuala ya Qur-an kuhakikisha Qur-an inakaa katika nyoyo za vijana ili jamii iweze kuwa bora na kuheshimiana wakubwa kwa wadogo.

Huku Muft Mkuu wa Tanzania Abubakari Zubeir amesema ni vyema watu wakajifunza Qur-an kwa sababu ni dawa ya kila tatizo, endapo waja wataifuata kwa mafunzo yaliyoamrishwa na kuacha yaliyokatazwa, kwani Qur-an imekataza kuuana, kuchukiana na kuvuruga amani.

Jumuiya ya kuhifadhisha Qur-an imetoa tuzo za heshima kwa wanaharakati wa Qur-an akiwemo Abdallah Basfar na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, huku ikitambua mchango huo kwa masheikh mbalimbali akiwemo Sheikh Ismail Mohammed, Sheikh Adam Ahmad, Marehemu Hashim Haji, Isihaka Abdehell, marehemu Yahya Hussein na Sheikh Mohammed.

Mashindano hayo yameanzishwa 1992 yakiwa yakimkoa na mpaka sasa ni mashindano ya kimataifa huku yakiwa niya 25 tangu kuanzishwa kwake.

(HABARI: HIRALY DAUDI/GPL)

Nishushe Idd Mosi… Roma Atawaongoza Wakali Hawa Kuliamsha Dude, Dar Live

Leave A Reply