The House of Favourite Newspapers

Mashindano ya Quran Afrika: Rais Mwinyi Ahimiza Kuhifadhi Quran Na Kufundisha, Mshindi ni Ibrahim Sow wa Ivory Coast (Picha +Video)

0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongea jambo katika fainali za 24 za Mashindano ya Quran Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al Hikma Foundation katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya kiislamu kuendelea kuhifadhi Quran Tukufu na kufundisha watoto wao kuisoma na pia wazidishe kutoa sadaka kwa watu wenye mahitaji hususani katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika fainali za 24 za Mashindano ya Quran Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al Hikma Foundation kwa kushirikisha nchi mbalimbali 22 za Afrika na nje ya Afrika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Machi 24, 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano na kuzidi kupiga hatua za maendeleo nchini.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameipongeza Taasisi ya Al Hikma Foundation kwa kuandaa mashindano hayo makubwa ambayo yanaitangaza Tanzania kwa kushirikisha nchi mbalimbali.

Mshindi wa kwanza wa Mashindano ya Quran Tukufu Afrika ni Ibrahim Sow wa Ivory Coast aliyepata shilingi milioni 27.

Pia ameipongeza Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kuyadhamini mashindano hayo kila mwaka.

Mshindi wa kwanza wa Mashindano hayo ni Ibrahim Sow wa Ivory Coast aliyepata shilingi milioni 27, mshindi wa pili Haafith Abdulkariim Kabiito kutoka Uganda shilingi milioni 17.2 , mshindi wa tatu Kamil Almin Swaleh kutoka Tanzania shilingi milioni 11.6 , mshindi wa nne Kamilou Koura kutoka Togo shilingi milioni 8.1 na mshindi wa tano Idris Nshimwe kutoka Burundi shilingi milioni 4.5

Mshindi wa pili wa Mashindano ya Quran Tukufu Afrika ni Haafith Abdulkariim Kabiito kutoka Uganda shilingi milioni 17.2.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akiwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir (kulia).

 

Leave A Reply